Home kimataifa MOURINHO MAMBO MAGUMU, KUKUTANA NA GUARDIOLA

MOURINHO MAMBO MAGUMU, KUKUTANA NA GUARDIOLA

 


KOCHA Mkuu wa Tottenham Hotspur,  Jose Mourinho ni miongoni mwa makocha ambao wapo kwenye orodha ya makocha ambao wapo katika presha ya kufutwa kazi.

Presha hiyo inatokana na mwendo mbovu ambao anakwenda nao na timu hiyo hivi karibuni baada ya kurithi mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya PSG.

Ikiwa leo jioni ataonja joto ya kichapo mbele ya Manchester City basi milango itazidi kufunguka kwa Mreno huyo kupigwa chini mazima.

Jumatano iliyopita alishuhudia timu yake ikitolewa kwenye Kombe la FA na Klabu ya Everton jambo ambalo limezidisha ugumu wa mambo.

Manchester City ni vinara wa Ligi Kuu England ikiwa watashinda leo wataongeza nguvu ya kutwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Liverpool. 

City ya Pep Guardiola imeshinda jumla ya mechi 15 mfululizo na kibindoni ina pointi 50 ikiwa imecheza mechi 22 imewazidi Spurs kwa pointi 14 ipo nafasi ya 8 na pointi 36.


SOMA NA HII  RONALDO KUIKOSA NAMBA YAKE MAZIMA UNITED, WOLVES YACHAPWA