Home Simba SC BAADA YA KUMALIZANA NA AS VITA KITUO KINACHOFUATA NI AL AHLY

BAADA YA KUMALIZANA NA AS VITA KITUO KINACHOFUATA NI AL AHLY


BAADA ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, leo kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea Bongo.

Bao pekee la ushindi kwa Simba lilipachikwa na mshambuliaji Chris Mugalu dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na Luis Miquissone dakika ya 59.

  Leo Februari 13 kikosi kinatarajia kuanza safari mchana ambapo kikosi pamoja na benchi la ufundi watapitia Ethiopia.

Kesho Jumapili, Februari 14 saa 6 mchana kitatua rasmi ardhi ya Bongo ili kuedelea na maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kimataifa.

Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kituo kinachofuata ni Al Ahly, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari 23, Uwanja wa Mkapa.


SOMA NA HII  OHOOO...YANGA MMEMSIKIA OKRAH HUKOO....BALAA LAKE MPAKA NABI ATAKUWA MWEKUNDU..