Home Habari za michezo OHOOO…YANGA MMEMSIKIA OKRAH HUKOO….BALAA LAKE MPAKA NABI ATAKUWA MWEKUNDU..

OHOOO…YANGA MMEMSIKIA OKRAH HUKOO….BALAA LAKE MPAKA NABI ATAKUWA MWEKUNDU..

Habari za Simba

Kiungo Mshambuliaji kutoka Ghana Augustine Okrah ameahidi makubwa endapo atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kitakashuka dimbani keshok Jumapili (Oktoba 23).

Simba SC itaalikwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kucheza dhidi ya Young Africans itakayokuwa mwenyeji wa mchezo huo, uliopangwa kuanza mishale ya saa Kumi na Moja jioni kwa Saa za Afrika Mashariki.

Okrah aliyesajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Bechem United ya nchini kwao Ghana, amesema yupo tayari kwa mchezo huo, na ameshiriki kikamilifu katika maandalizi ya kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa Mashabiki wa Soka nchini Tanzania.

“Kikubwa nahitaji kwenda kushindana zaidi ya wapinzani walivyo, kucheza kwa malengo ya timu ili kupata ushindi ambao utatuweka kileleni mwa ligi kwa uhakika zaidi, kutokana na ubora wa kikosi chetu kwa sasa hilo linawezekana.” amesema Okrah

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana Agosti 13, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Young Africans ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Simba yenye alama 13 sawa na Young Africans, ndio kinara wa ligi hiyo lakini ikiwa na moto baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  DALALI AINGILIA KATI ISHU YA UBINGWA SIMBA...ADAI WAMESHIKIWA NAFASI ...ATOA ONYO HILI...