Home news DALALI AINGILIA KATI ISHU YA UBINGWA SIMBA…ADAI WAMESHIKIWA NAFASI …ATOA ONYO HILI…

DALALI AINGILIA KATI ISHU YA UBINGWA SIMBA…ADAI WAMESHIKIWA NAFASI …ATOA ONYO HILI…


LICHA ya Yanga kuongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya alama tano, aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, amesema kuwa Yanga imewashikia kwa muda tu nafasi yao.

Yanga kwa sasa wako kileleni mwa ligi kuu wakiwa na pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 14 ambapo wameshinda mechi 11 na sare tatu.

Simba wao wamecheza mechi 15, wameshinda tisa, sare nne na kupoteza mbili wako nafasi ya pili na alama zao 31.

Dalali alisema kuwa: “Kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu Bara hilo halina ubishi wale wenzetu wametushikia nafasi yetu na muda utakapowadia tunakwenda kuwashusha na safari ya ubingwa itaanzia hapo, kikubwa tuwe wamoja tusitengeneze makundi ambayo yatakuja kutuvuruga na tukatoka kwenye malengo yetu.”

SOMA NA HII  MECHI 3 TU, YANGA YACHANA MKATABA WA MAXI, PIA YAMUITA BEKI KITASA........., GAMONDI AANZA KUTAFUTA REKODI