Home news BAADA YA KUPIGWA 7-0 JANA..MASAU BWIRE AIBUKA NA SABABU HIZI…ADAI WANAMAJONZI YA...

BAADA YA KUPIGWA 7-0 JANA..MASAU BWIRE AIBUKA NA SABABU HIZI…ADAI WANAMAJONZI YA MSIBA WA SONSO…


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amekiri kuwa mnyonge, kufuatia timu yao kukubali kichapo cha mabao 7-0, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Hatua ya 16 Bora dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC.

Ruvu Shooting ilikua mwenyeji wa Mchezo huo jana Jumatano (Februari 16), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho cha aibu tangu msimu huu 2021/22 ulipoanza.

Masau Bwire amesema matokeo hayo sio rafiki kwa afya, kwa yoyote anayehusika na Ruvu Shooting, kwani yameumiza nyoyo zao na kuwatia majonzi makubwa.

Amesema hawakutarajia kukutana na matokeo ya namna hiyo, kutokana na kikosi chao kilivyojiandaliwa kwa zaidi ya juma moja, lakini kilichotokea jana Jumatano (Februari 16) hawana budi kukubaliana nacho kwa sababu ndio matokeo ya mchezo wa soka.

“Imenitia simanzi sana mimi, naamini hata kwa wengine wanaohusiska na timu hii wana uchungu wa kupoteza mchezo huu kwa kiasi kikubwa cha mabao, tunapaswa kukubaliana na matokeo haya, lakini yanaumiza sana,” amesema Masau Bwire

Hata hivyo Masau Bwire kuna sababu ambazo anaamini zilimepeleka kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 7-0 na Simba SC ambayo imeanza kuamka kutoka usingizini.

Jambo la kwanza ambalo Masau amelitaja ni Majonzi ya kufiwa na mchezaji wao Ally Mtoni Sonso, ambaye alifariki dunia mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam.

Lingine ni Dharau ambayo anaamini iliwavaa Wachezaji wao ambao walihisi wangeimudu Simba SC kwa urahisi, hasa baada ya kuona madhaifu yao katika michezo kadhaa iliyopita, hivyo walijitoa na kucheza soka la kufunguka na ambalo lilitoa nafasi kwa wapinzani kupata ushindi mkubwa.

Kwa matokeo hayo Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ikiungana na Pamba FC, Young Africans, Coastal Union, Azam FC, Polisi Tanzania, Kagera Sugar na Geita Gold FC.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- KUSHANGILIA YANGA KUPANGWA NA MAMELOD NI AIBU KWETU....