Home Uncategorized NAMUNGO WANA JAMBO LAO KWA WANA ARUSHA, KUTAMBULISHA MAJEMBE MAPYA MATATU

NAMUNGO WANA JAMBO LAO KWA WANA ARUSHA, KUTAMBULISHA MAJEMBE MAPYA MATATU


 UONGOZI wa Namungo FC, umeweka wazi kuwa ndani ya wiki hii wamepanga kuwafanyia sapraizi mashabiki wake waliopo Arusha kwa kutambulisha nyota watatu wapya kabla ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Namungo FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery itamenyana na Simba, Agosti 30 kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6.


Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Ofisa Habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia, ameliambia Spoti Xtra kuwa:“Tumewaandalia sapraizi ya kutosha Wanaarusha, tutawatambulisha wachezaji wapya watatu, pia jezi tutakazotumia msimu wa 2020/21. Kikubwa watu wajitokeze siku ya mechi kutuunga mkono. 


Dirisha la usajili lilifunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.Miongoni mwa nyota wapya ambao tayari wametambulishwa na Namungo ni pamoja na Shiza Kichuya,Sixtus Sabilo,Stephen Sey.

SOMA NA HII  BARCELONA BADO INA HESABU ZA KUINASA SAINI YA NEYMAR