Home Habari za michezo WAKATI MASTAA SIMBA WAKITAMBA…MAYELE KAWASIKILIZA WEE….KISHA ‘SIMPO’ TU KAWAJIBU HIVI…

WAKATI MASTAA SIMBA WAKITAMBA…MAYELE KAWASIKILIZA WEE….KISHA ‘SIMPO’ TU KAWAJIBU HIVI…

Habari za Yanga

Yanga iko kambini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao Simba, huku Fiston Mayele akisema kwa kauli pana kwamba; ‘“Acheni waje”. Wachezaji wa timu hiyo wamejutia matokeo ya mengi iliyopita na wamesisitiza kurudisha heshima yao kupitia mchezo wa dabi.

Mastaa wa Yanga wameonyesha kujutia hatua ya kutolewa Ligi ya Mabinghwa Afrika mbele ya Al Hilal ya Sudan na sasa wanajipanga upya kabla ya kutua kujiuliza katika hatua nyingine ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia mapema mwezi ujao.

Inafahamika kwamba mastaa wakubwa wamewatumia mabosi wao ujumbe wa kuomba radhi kwa kilichotokea, lakini wakatoa tamko zito kuhakikisha wanashinda mchezo wa Jumapili.

Akizungumza Mayele alisema baada ya mchezo wa ugenini na Al Hilal walikutana wachezaji wote na kufanya kikao chao wenyewe kuangalia wapi walipokosea na wanatakiwa kufanya nini kwenye michezo ijayo ili kupata matokeo bora.

Mayele alisema baada ya kikao kila mmoja aliondoka akiwa na hamu ya kubadilisha matokeo mabaya waliyopata kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kurudisha ubora, muendelezo wa matokeo mazuri kwenye kikosi chao kama ilivyokuwa mwanzo wa msimu huu.

“Kila mchezaji atakayepata nafasi ya kucheza kwenye mechi inayofuata atakwenda kujituma zaidi ya ilivyokuwa kwenye mechi iliyopita kwani hiyo ni silaha ya kufanya vizuri kama malengo yetu yalivyo na tulivyo kubaliana wenyewe ndani ya kikao chetu,” alisema Mayele aliyefunga mabao matatu kwenye Ligi na kumaliza na mabao saba katika Ligi ya Mabingwa na kuongeza;

“Baada ya kumaliza mechi ya mashindano ya CAF, tumerejea nyumbani jinsi gani tutacheza dhidi ya Simba, mechi itakuaje, tumejipangaje hayo yote maandalizi yake ndio yameanza sasa. Hakuna mchezo dhidi ya Simba uliyowahi kuwa rahisi ila lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunafanya vizuri, ndio maana tunasema waacheni waje tuwaonyeshe.”

Kabla ya mchezo wa Jumapili amekutana na Simba mara tano, hajafunga bao lolote wakati michezo miwili ya Ngao ya Jamii, ameitungua timu hiyo mabao matatu kwenye michezo yote miwili.

Wakati Mayele akuitamba hiyo na wenzeka, Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said alisema; “Hakuna mafanikio ambayo yamepatikana kwa usiku mmoja, kujenga ni hatua ngumu na kufikia mafanikio unatakiwa kupitia hatua mbalimbali tofauti,tumesikitika kwa hatua hii ya kutolewa Ligi ya Mabingwa lakini bado tuko imara,”alisema Hersi.

“Hata wachezaji wetu wameumizwa na hili wapo ambao nimezungumza nao na wengine hata kuandika ujumbe wa kuomba radhi na sasa wanajua kwamba wamewaangusha mashabiki wao lakini wanataka kutafuta nguvu mpya ya kurejesha imani yao kwa mashabiki wao na hii itaanzia sasa kuanzia mchezo wetu ujao dhidi ya Simba.” Yanga kwa sasa wameelekeza nguvu zao kushinda dabi pamoja kufuzu makundi ya Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  YAMETIMIA ...CHICO USHINDI AFYEKWA YANGA....YACOUBA SOGNE NAYE KUPITISHIWA PANGA LA MOTO JUMLA JUMLA...