Home Habari za michezo GENK BADO WANAKUMBUKA MAAJABU HAYA YA SAMATA

GENK BADO WANAKUMBUKA MAAJABU HAYA YA SAMATA

samata

Nahodha wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta ameendelea kuenziwa na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa jezi yake maalum kuuzwa katika maduka ya timu hiyo.

Samatta ambaye ni Legend wa timu hiyo amewekwa katika kundi la wachezaji watano wa kikosi hicho waliowahi kupita na kufanya mambo makubwa.

Katika duka la kuuzia vifaa vya michezo la timu hiyo kuna jezi maalum iliyotengenezwa na kuuzwa katika duka hilo, moja ya jezi inayouzwa ni pamoja na jezi ya Samatta yenye picha yake akiwa anafunga kwa kichwa katika mechi ya Genk na Liverpool.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA....BOSI SportPesa AIBUKA NA HAYA....ADAI WALIFURAHI KUACHANA NAO...