Home kimataifa RONALDO KUIKOSA NAMBA YAKE MAZIMA UNITED, WOLVES YACHAPWA

RONALDO KUIKOSA NAMBA YAKE MAZIMA UNITED, WOLVES YACHAPWA


DILI la nyota wa Juventus ambaye tayari ameshawaaga mabosi wake pamoja na mashabiki Cristiano Ronaldo likijibu ndani ya Manchester United hataweza kuvaa namba yake pendwa mgongoni ile namba 7 kutokana na sheria za Ligi Kuu England.

 Kwa sasa dili la Ronaldo na Manchester United limefika sehemu nzuri kwa kuwa wakati wowote nyota huyo anafanyiwa vipimo na kupewa dili la miaka miwili.

 Ikumbukwe kwamba jezi namba 7 alikuwa akiivaa alipokuwa ndani ya United kabla ya kusepa msimu wa 2009 kwa kuwa imesajiliwa kuvaliwa na Edinson Cavani.

Huenda akavaa kati ya jezi namba 12,15,24,30,31,33 na 35 kwa kuwa zipo wazi. Sheria ya Premier League inaeleza kuwa kabla ya msimu kuanza kila klabu huwasilisha jezi namba ya kila mchezaji wa kikosi cha kwanza na namba anaweza kupewa mchezaji mwingine endapo yule wa awali ataondoka na kwa sasa Cavan bado yupo Manchester United.

Hivyo namba hiyo Ronaldo anaweza kuitumia msimu ujao ikiwa bado ataendelea kuwa ndani ya United na dili lake likajibu kwa wakati huu.

Mashabiki kwa sasa wanamsubiria kwa shauku kubwa nyota huyo huku wakiwa na furaha pia ya ushindi wao wa mchezo wa jana mbele ya Wolves baada ya ubao wa Uwanja wa Molineux kusoma Wolves 0-1 Manchester United.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Mason Greenwood ilikuwa dakika ya 80.


SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED BADO WANAAMINI WATAMPATA HAALAND