Home Uncategorized ISHU YA MZAMBIA KUIBUKIA NDANI YA SIMBA IMEKAA NAMNA HII

ISHU YA MZAMBIA KUIBUKIA NDANI YA SIMBA IMEKAA NAMNA HII

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba hauna mpango wa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Klabu Orlando Pirates, Justin Shonga raia wa Zambia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Zambia amekuwa akitajwa kuingia rada za Simba ili akaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Safu ya ushambuliaji ndani ya Simba inaundwa na nyoa wanne ambao ni John Bocco, Meddie Kagere, Charles Ilanfya na Chris Mugalu.

Ambapo kwa hao wanne ni wawili wenye uhakika wa kuanza kikosi ambao ni Kagere na Bocco, Mugalu yeye majeruhi yamekuwa yakimuweka benchi huku Ilanfya akiwa hayupo kwenye mpango wa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck. 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mpango wa kusajili kwenye dirisha dogo upo ila sio kwa Shonga. 

“Hatuna mpango wa kumsajili Justin Shonga kwa kuwa hayupo kwenye orodha ya wachezaji ambao tunawahitaji kwa sasa.

“Mpango wa kusajili ndani ya timu ya Simba upo ila utawekwa wazi hivi karibuni, kwa sasa kuna kamati maalumu ambayo inashughulikia hayo masuala” .

Shonga rekodi zake zinaonyesha kuwa ndani ya Klabu ya Orlando Pirates amecheza jumla ya mechi 46 na ametupia mabao 10.

Pia kwenye timu yake ya taifa ya Zambia amecheza jumla ya mechi 24 na ametupia mabao 13.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUFUTWA KWA LIGI KUU BARA