Home Habari za michezo TANZANIA YAZIDI KUPAA KIMATAIFA…FIFA WAIPANGA NA UFARANSA KOMBE LA DUNIA…RATIBA NZIMA IKO...

TANZANIA YAZIDI KUPAA KIMATAIFA…FIFA WAIPANGA NA UFARANSA KOMBE LA DUNIA…RATIBA NZIMA IKO HIVI..


Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 ‘Serengeti Girls’ imepangwa kundi D Kombe la Dunia litakalofanyika nchini India kuanzia Oktoba 11 mpaka 30 mwaka huu.

Droo ya Kombe la Dunia ilipangwa jana mchana na Tanzania imewekwa kundi moja sambamba na Japan, Canada na Ufaransa.

Serengeti Girls ilifuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kuifunga Cameroon jumla ya mabao 5-1 baada ya raundi ya kwanza mchezo uliochezwa Yaounde, Cameroon kushinda 4-1 na wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Serengeti ilishinda 1-0 bao likifungwa na Neema Paul Kinega.

Makundi mengine katika Kombe hilo, kundi A India, USA, Morocco na Brazili, Kundi B Ujerumani, Nigeria, Chile na New Zealand.

Kundi C Spain, Colombia, Mexico na China PR.

SOMA NA HII  NTIBANZONKIZA AANZA MAJAMBOZI GEITA GOLD...SHIZA KICHUYA NAYE YUMO...