Home news MAKAME AANIKA MAISHA YA SIRI YA ‘FEI TOTO’…ADAI ANAPENDA KUOMBAOMBA KILA KITU…WALIKUWA...

MAKAME AANIKA MAISHA YA SIRI YA ‘FEI TOTO’…ADAI ANAPENDA KUOMBAOMBA KILA KITU…WALIKUWA WANAMCHEKA…


UMAARUFU alionao kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ haujaja kwa bahati mbaya bali ni jambo alilojitabiria tangu akiwa na umri mdogo mbele ya marafiki wake.

Beki wa Namungo, Abdulaziz Makame ‘Bui’ ni kati ya mashuhuda wa maneno ya Fei aliyosema miaka mingi iliyopita kuwa, atakuja kuwa na jina kubwa ndani na nje.

Bui alisema Fei Toto alikuwa na kipaji tangu akiwa mtoto, kipindi hicho wakicheza mtaani watu wengi walikuwa wanakusanyika kumtazama anavyocheza.

“Kama kuna neno nalikumbuka ambalo Fei aliongea kipindi tukiwa wadogo, ingawa mimi ni mkubwa kidogo kwake, alisema nitakuja kuwa staa mkubwa sana, tukawa tunacheka, tukijua ni maneno ya kitoto.” alisema Makame na kuongeza;

“Kauli yake imetimia jina lake limekuwa kubwa, naamini akiamua kwenda kucheza nje basi atakamilisha ndoto zake ambazo alikuwa anasema atakuwa staa ndani na nje.”

Alibainisha kipaji cha Fei kilikuwa kinavutia tangu akicheza mtaani, kutokana na namna wachezaji wenzake walivyokuwa wanapenda aanzishwe kwenye kila mechi.

Alisema baada ya Fei kusajiliwa Yanga, alifurahia na kuona anakwenda kuishi ndoto zake.

“Nje na soka kitu ambacho Fei alikuwa ananichekesha alikuwa anapenda kulakula sana, ukishika kitu anakwambia kaka naomba, kiukweli tumetoka mbali nikikumbuka huwa nacheka sana.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...BENCHIKHA 'KUUWA MENDE KWA NYUNDO'....