Home news PAMOJA REKODI NZURI YA SIMBA DHIDI YA IBENGE….PABLO AINGIA UBARIDI…AFUNGUKA WASIWASI WAKE…

PAMOJA REKODI NZURI YA SIMBA DHIDI YA IBENGE….PABLO AINGIA UBARIDI…AFUNGUKA WASIWASI WAKE…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema licha ya changamoto kadhaa walizopitia ila amefurahishwa na morali ya timu yake kuelekea mchezo wa Jumapili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco, huku rekodi tamu ikiibeba timu hiyo dhidi ya Kocha Florent Ibenge anayeinoa Berkane.

Timu hizo zinakutanakatika mchezo wa tatu wa Kundi D, huku Simba ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Niger, wakati wenyeji wao wakitoka kupasuka mabao 3-1 na Asec Mimosas, lakini kocha Pablo akichekelea morali ya wachezaji wake ilivyo kwa sasa.

“Kwa siku mbili hatukufanya mazoezi kwa sababu ya safari ndefu kutoka Afrika, Ulaya kisha Afrika tena ila nimefurahishwa na morali ya wachezaji, kwani wameahidi kupambana kwa ajili ya timu yao.” alisema Pablo.

Licha ya Pablo kujazwa upepo na mastaa wake, lakini rekodi ya Simba dhidi ya Kocha wa sasa wa RS Berkane, Florent Ibenge inawaongezea mzuka zaidi kwani katika mechi nne walizokutana kipindi akiwa na AS Vita, kocha huyo alipasuka mara tatu na kushinda mchezo mmoja tu.

Licha ya rekodi hizo tamu ambazo Simba ilikutana na Ibenge katika Ligi ya Mabingwa Afrika ndani ya misimu mitatu iliyopita, bado haijamtia kiburi Kocha Pablo alisema anaendelea klukiandaa kikosi ili kuipa timu hiyo ushindi mwingine katika kundi hilo. Katika mechi hizo nne, Simba ilipasuka kwa Ibenge mabao 5-0, lakini ikishinda 2-1 katika makundi ya msimu wa 2018-2019 kisha 1-0 na 4-1 msimu uliopita wa 2020-2021, ikivuna mabao saba na kufungwa pia saba. Pia ilishakutana mra moja kwenye michuano yua Kagame mwaka 2012 na timu hizo kutoka sare ya 1-1.

“Kikubwa ni maandalizi mazuri yatakayotuwezesha kupata ushindi, hayo mengine yapo tu ila hayana nafasi kubwa kwa sababu mazingira nayo hubadilika kwani kipindi hicho aliifundisha AS Vita na sasa Berkane,” alisema Pablo.

Simba ndio kinara wa kundi D ikiwa na pointi nne, ikishinda dhidi ya Asec Mimosas kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 13, kisha kufungana bao 1-1, na Gendarmerie Nationale Februari 20, huku ikifuatwa kwa karibu na RS Berkane na Aserc zenye pointi tatu kila moja na USGN ikishika mkia na alama moja tu, kwani ilifungwa mechi yao ya kwanza na Berkane kwa mabao 5-3 kuisha kudroo na Simba.

SOMA NA HII  KUHUSU ULE MPANGO WA KUSAJILIWA NA YANGA....KAMBOLE KAANIKA YOTE WAZI..."LAKINI NAKUJA...."