Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…SIMBA WAIBA ‘UPUPU’ WA ZAMALEK…MATOLA AKOLEZA MOTO…BARBARA ATOA TAMBO…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…SIMBA WAIBA ‘UPUPU’ WA ZAMALEK…MATOLA AKOLEZA MOTO…BARBARA ATOA TAMBO…


SIMBA inajiandaa kuivaa Berkane kwenye pambano lao la Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho, lakini juzi usiku β€˜iliibia’ mbinu za kivita kutoka kwa Zamalek ya Misri waliokutana nao mazoezini kabla ya makocha wa timu hizo Pablo Franco wa Simba na Patrice Carteron wa Zamalek waliteta pamoja ili kubadilishana mawazo kabla ya timu hizo kushuka uwanjani wikiendi hii kuvaana na RS Berkane na Wydad Casablanca zote za Morocco.

Simba ilitua Casablanca juzi saa 9 alasiri na jioni ikafanya mazoezi ya muda wa saa 1:15, lakini kabla ya kupiga tizi kwenye Uwanja wa Palmeraie Country Club, ilipoikuta Zamalek ikijifua pia, hivyo kuisubiri wakiingalia inavyopeana mbinu za kiufundi, kisha makocha hao kusalimiana na kupiga stori mbili tatu, ikielezwa walikuwa wakifahamishana mbinu za kutoka na ushindi nchini humo.

Simba ilifanya mazoezi yake kuanzia saa 2 usiku za Morocco ambazo ni sawa saa 4 usiku za Tanzania ili kuiweka miili ya nyota wake ikiwa sawa baada ya safari ndefu kutoka Dar es Salaam hadi Niamey, Niger na kutoka Niger hadi Uturuki kisha Morocco kwa ajili ya mechi yao ya Jumapili dhidi ya RS Berkane katika mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwenye mazoezi ya kwanza walifanya ya nguvu kama kuruka koni, kukimbia mbio ndefu na fupi yalikuwa yanasimamiwa na kocha wa viungo, Daniel De Castro wakati kocha mkuu akibadilishana mawazo na kocha wa Zamalek, aliyetimka baadaye na timu hiyo inayoshiriki makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kesho itavaana na Wydad.

Baada ya hapo walipiga tizi la mbinu za kukaba kutokana na wapinzani wao RS Berkane walivyo, huku pia wakishambulia kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mipira ya pembeni.i.

Kwa jana nyota wa Simba walianzia gym ili kutafuta stamina kabla ya jioni kurudi tena uwanjani kwa mazoezi mengine, huku kocha Msaidizi Seleman Matola akifichua wanaendelea kuyafanya mazoezi mepesi ya mbinu ili kulinda utimamu wa wachezaji kabla ya kusafiri hadi Berkane mji uliopo kilomita zaidi ya 600 kutoka Casablanca kwa ajili ya mechi yao wa Jumapili utakaopigwa saa 4 usiku katika Uwanja wa Manispaa ya Mji wa Berkane.

SOMA NA HII  WAKATI MKIZANI SIMBA IMEKWISHA ...PABLO AMEWATAZAMAA WEE..KISHA KAIBUKA NA NENO HILI MOJA TU...

Mara kikosi kikifika Berkane kitajifua usiku na  kitamalizia programu kwenye uwanja utakaotumiwa kwa mchezo huo ulioshuhudiwa wiki iliyopita, ukizalisha mabao nane, Berkane ikishinda mabao 5-3 dhidi ya USGN.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema kikosi hicho kinaendelea vizuri na maandalizi kwani wamepata muda wa kutosha kujiandaa kulingana na vile ambavyo benchi la ufundi lilihitaji.