Home news BAADA YA KUMUONA MAYELE ‘ANAVYOTETEMA’….KIIIZA ‘AKUNJA MDOMO’ KISHA AKASEMA HAYA..

BAADA YA KUMUONA MAYELE ‘ANAVYOTETEMA’….KIIIZA ‘AKUNJA MDOMO’ KISHA AKASEMA HAYA..


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ambaye hivi sasa anacheza Kagera Sugar, Mganda, Hamis Kiiza ‘Diego’amemuangalia straika waYanga, Mkongomani, Fiston Mayele na kutamka kuwa jamaa anajua huku akimtabiria makubwa katika timu hiyo.

Kiiza aliyewahi kuichezeaYanga kabla ya kwenda Simba, alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yaYanga dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulimalizika kwaYanga kushinda mabao 3-0 yakifungwa na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’na Mayele aliyepachika mawili.

Kiiza ambaye aliwafunga Simba katika mchezo wa ligi, alisema kuwa kwa aina ya uchezaji na mfumo ambao wanautumiaYanga, mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi msimu huu.

Kiiza alisema kuwaYanga mashambulizi yao wanayafanya kutokea pembeni wakiwatumia mabeki wa pembeni na mawinga kupiga krosi ambazo ndiyo zinamrahisishia Mayele kufunga mabao.

Aliongeza kuwa uzuri wachezaji wote wa Yanga wanamjua vizuri Mayele, hivyo wanatumia mipira ya krosi katika kumpa mipira hiyo ambayo inazaa mabao.

“Kwa aina ya uchezaji na kimbinu wanayotumia wachezaji wenzake kumchezesha Mayele, basi namtabiria kufanya mengi mazuri katika msimu huu ikiwemo kutwaa ufungaji bora.

“Yanga mashambulizi yao wanayatumia kupitia pembeni kwa maana ya kupiga krosi ambazo zote wanampigia Mayele, ni kitu ambacho wanaonekana kukifanyia kazi mazoezi.

“Mabao yote aliyotufunga Mayele yametokea pembeni moja la krosi na lingine la faulo iliyotokea pembeni ambayo yote yakifungwa kwa kichwa,” alisema Kiiza.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAMBA KUPATA MAFAILI MUHIMU YA AL AHLY