Home news BAADA YA KUMUONA HANA JIPYA…NABI ASHINDWA KUMVUMILIA MAKAMBO…AMLIPUWA…ADAI HAYUKO SAWA…

BAADA YA KUMUONA HANA JIPYA…NABI ASHINDWA KUMVUMILIA MAKAMBO…AMLIPUWA…ADAI HAYUKO SAWA…


KWA mara ya kwanza Kocha Mkuu waYanga, Mtunisia Nasreddine Nabi ameibuka na kutaja sababu inayomfanya mshambuliaje wake Heritier Makambo kushindwa kufunga mabao.

Nyota huyo ameonekana kutokuwa na msimu mzuri kwake kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Tangu kuanza kwa msimu huu mshambuliaji huyo hajafanikiwa kufunga bao katika ligi huku akipata ugumu wa namba kutoka kwa Mkongomani mwenzake, Fiston Mayele aliyekuwepo katika ubora mkubwa.

Akizungumza  mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Nabi alisema ukame wa mabao unamfanya atoke mchezoni, apoteze umakini na kujikuta kukosa nafasi nyingi za wazi za kufunga.

Nabi alisema kuwa mshambuliaji huyo anatakiwa kutuliza akili yake na kupunguza presha anayoipata kutoka kwa mshambuliaji mwenzake Mayele mwenye mabao tisa katika ligi.

Aliongeza kuwa anaamini kama akituliza akili zake, basi atafunga idadi kubwa ya mabao kutokana na kiwango kizuri alichonacho hivi sasa ambacho anakionyesha uwanjani.

“Kisaikolojia Makambo hayupo sawa, hiyo ni kutokana na presha kubwa anayoipata kutoka kwa mshambuliaji mwenzake Mayele aliyekuwa katika kiwango bora hivi sasa.

“Hiyo inaweza kumkuta mchezaji yeyote mwenzake anapofanya vizuri pale anapopata nafasi ya kucheza, Makambo anatakiwa kupunguza presha itakayomfanya acheze kwa kujiamini.

“Siku zote mshambuliaji unapopoteza nafasi za wazi za kufunga, hali ya kujiamini inapungua na kujikuta mchezaji akitumia vibaya nafasi ya kufunga kama ilivyokuwa kwa Makambo ambaye leo (Jumapili) tulipocheza dhidi ya Kagera alishindwa kutumia nafasi zaidi ya moja za wazi za kufunga, hiyo imetokana na presha aliyokuwa nayo hivi sasa anatamani kufunga lakini anashindwa kutokana na kupania,” alisema Nabi na kuongeza kuwa.

“Ninaamini atatulia na kucheza vizuri ikiwemo kufunga mabao mara baada ya kumtengeneza kisaikolojia, kama kocha hilo ndiyo jukumu langu nitajitahidi kumbadilisha na kumuweka sawa.”

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA ZANACO, KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI