Home Habari za michezo KISA KUITWA TIMU YA TAIFA TENA…BANDA AAMUA KULIAMSHA NA HILI…’AJIMIMINIA MINYAMA’…

KISA KUITWA TIMU YA TAIFA TENA…BANDA AAMUA KULIAMSHA NA HILI…’AJIMIMINIA MINYAMA’…

Habari za Michezo

Mlinzi wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Abdi Banda amekiri kufurahishwa kurejea tena kwenye kikosi hicho baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Banda ambaye anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini amesema muda wote yupo tayari kuitumikia timu ya taifa pale atakapohitajika.

“Mimi sio mchezaji wa kusema lazima niitwe timu ya taifa, ninaitwa timu ya taifa kama labda mwalimu ananihitaji kama mwalimu hanihitaji basi sioni ulazima wa kuitwa”, amesema Banda.

Nyota huyo wa Zamani wa Simba anajivunia rekodi za kipekee akiwa na kikosi cha Taifa Stars na anatamani kuendelea kuzilinda rekodi hizo.

“Kitu ambacho ninafurahi ni kwamba sijawahi kupoteza mchezo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hii ni rekodi yangu” amesema Banda.

Abdi banda alijumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger na kutanguliza mguu mmoja kwenye michuano ya mataifa ya Afrika ‘Afcon’ itakayofanyika mwakani nchini Ivory coast.

SOMA NA HII  WAKATI HABARI YA MJINI NI 'MZUNGU' NA AZIZ KI....KIRAKA WA TZ PRISONS KAWATAZAMA WEE...KISHA AKAIBUKA NA HILI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here