Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YAKE YA KUTUA YANGA …NOVATUS AIBUKA NA HILI…AMTAJA DICKSON JOB….

KUHUSU ISHU YAKE YA KUTUA YANGA …NOVATUS AIBUKA NA HILI…AMTAJA DICKSON JOB….

Tetesi za Usajili Yanga SC

Kiraka wa Taifa Stars na Zulte Waregem ya nchini Ubelgiji Novatus Dismas amesema kucheza Dabi ya Watani wa Kariakoo kwake haitakuwa na maana kama hana maisha mazuri.

Akizungumza kupitia Redio ya Clouds FM. Novatus anasema

“Kwa namna fulani na-miss kucheza derby ya Simba na Yanga kwa sababu nikiangalia vijana wenzangu ambao nimechezanao wapo kwenye hizo timu [Job, Kibwana] nafikiri ni mechi ambayo matokeo yake hayafikiriki.”

“Lakini sioni kama nahitaji kucheza derby (Kariakoo derby) kama sina maisha mazuri kwa hiyo napambana kutengeneza maisha mazuri halafu derby itakuja tu.”

“Nikiwa mdogo nilikuwa naamini nina kipaji na uwezo mzuri wa kucheza mpira lakini sikuwahi kuwaza kama ipo siku nitacheza Ulaya kwa hiyo sikushangaa sana kupata nafasi ya kwenda Ulaya kwa sababu tayari nilikuwa najua nina uwezo mzuri.”

“Wazazi wengi wa kitanzania huwa hawaamini vijna kufanikiwa kupitia michezo lakini kwa sasa mambo yamebadilika na wazazi wengi wamebadilika kulingana na fursa ambazo wachezaji wanazipata na jinsi ambavyo mpira wa Tanzania umekua.”

SOMA NA HII  WAARABU WAMFANYIA KUFRU RONALDO...KULIPWA MSHAHARA BIL 40 KWA MWEZI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here