Home Uncategorized MWADUI FC HAWAJAKATA TAMAA, WAITAKA 10 BORA

MWADUI FC HAWAJAKATA TAMAA, WAITAKA 10 BORA


 LICHA ya kuanza kwa kusuasua ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kuyeyusha pointi tisa kwenye mechi tatu za mwanzo Kocha Mkuu wa Mwadui, Khalid Adam amesema kuwa wanahitaji kumaliza ligi wakiwa ndani ya 10 bora.

Mwadui iliyomaliza ligi msimu wa 2019/20 ikiwa nafasi ya 11 na pointi zake 47 msimu huu ipo nafasi ya 17 ikiwa imecheza mechi tatu na haijaambulia pointi.


Ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United kisha ikakutana na kichapo cha bao 1-0 mbele ya Dodoma FC na mabao 2-1 mbele ya KMC.

Akizungumza na Spoti Xtra, Adam alisema kuwa ni mwanzo wa ligi ushindani huwa mkubwa na kupoteza kwao mechi hizo hakujawatoa kwenye ramani.

“Msimu uliopita tulikosa pointi moja pekee ili kumaliza ligi tukiwa ndani ya 10 bora, kwa sasa ligi ndo inaanza kupoteza mechi za mwanzo haina maana kwamba tutapoteza kila kitu ligi bado inaendelea na mechi zipo nyingi,” alisema Adam. 

Mwadui ina kibarua cha kumenyana na Ihefu FC iliyotoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, Septemba 27 majira ya saa 10:00 jioni, Uwanja wa Mwadui Complex.

 

SOMA NA HII  BARCELONA YATINGA 16 BORA BILA MESSI