Home Uncategorized MBADALA WA KEPA NDANI YA CHELSEA ASAINI DILI LA MIAKA MITANO

MBADALA WA KEPA NDANI YA CHELSEA ASAINI DILI LA MIAKA MITANO




 Chelsea imekamilisha usajili wa mlinda mlango Edouardo Mendy kutoka klabu ya Rennes ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitano.

Nyota huyo anakuwa ni wa saba kusajili ndani ya Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu Frank Lampard ambaye alikuwa anahitaji saini ya kipa ambaye atasaidiana na Kepa Arrrizabalaga ambaye amekuwa akifanya makosa kwenye mechi za hivi karibuni.


Kipa huyo mwenye miaka 28 dau lake ni Euro milioni 22 ambapo aliweza kutimiza majuku yake ndani ya Rennes kwa kuweza kufuzu katika Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza msimu uliopita, na klabu hiyo ya Ufaransa ilishika nafasi ya tatu kwenye Ligue 1 na anakuwa kipa wa pili kujiunga na Chelsea kutoka Rennes baada ya Petr Cech.


Msimu uliopita baada ya kucheza mechi 38 ndani ya Ligi Kuu England, Chelsea iliruhusu kufungwa jumla ya mabao 54 jambo lililomfanya kocha huyo kumtafuta mbadala wake licha ya kwamba atabaki kuwa kipa namba moja.

Mendy amesema:”Ninafuraha kubwa kujiunga na Chelsea ninaamini tutafanya kazi kwa kushirikiana.”
SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ACHARUKA, AMTAJA AKAPOMBE - VIDEO