Home Uncategorized KMC YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

KMC YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

 


UONGOZI wa KMC umesema kuwa unazihitaji pointi tatu kesho, Septemba 25 mbele ya Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime ili kuendelea kuwa vinara ndani ya ligi.

KMC kwa sasa ipo Bukoba yalipo makao makuu ya Kagera Sugar itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibamiza mabao 2-1 Mwadui FC huku Kagera Sugar ikitoka kupoteza mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha wa KMC Habib Kondo amesema kuwa wapo tayari kuendeleza rekodi zao za kupata ushindi ndani ya ligi.

“Mashindano ni vita.Na siku zote matayarisho bora ni silaha kubwa sana itakayoleta matokeo mazuri na ya kupendeza. Sisi hatuwahofii Kagera kwa kuwa tunaimani na uwezo ambao vijana wetu wanao wakutupatia matokeo yatakayo tubakisha nafasi ya kwanza ndani ya ligi.”

Naye Ofisa Habari  KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanajitahidi kadiri wawezavyo kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri katika mechi zao hivyo wadau waendelee kuwapa sapoti.

 


SOMA NA HII  MSHAHAMBULIAJI YANGA APATA DILI RWANDA