Home Uncategorized CHEKI RATIBA YA LIGI KUU BARA MECHI ZA MWANZO RAUNDI YA NNE

CHEKI RATIBA YA LIGI KUU BARA MECHI ZA MWANZO RAUNDI YA NNE


KESHO ni mwanzo wa raundi ya nne baada ya tatu kukamilika kwa mechi tisa kupigwa huku moja pekee ikiambulia sare tasa.


Jumla yalifungwa mabao 14 kwa mzunguko wa tatu kwa msimu huu ambao umekuwa na ushindani mkubwa mwanzo.

 Septemba 25, Ijumaa mambo yataendelea ndani ya Ligi Kuu Tazania Bara ikiwa ni mwanzo wa raundi ya nne kwa msimu wa 2020/21 mechi zake zipo hivi:-


Kagera Sugar ikiwa imetoka kupoteza mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga Uwanja wa Kaitaba itabaki hapohapo na itawakaribisha KMC majira ya saa 8:00 mchana.

KMC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi tisa kibindoni na wamefunga mabao nane wametoka kushinda mabao 2-1 mbele ya Mwadui FC walipokutana pale Mwadui Complex, Shinyanga.


Mbeya City wataendelea kubaki pale Sokoine wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam FC, wanawakaribisha Namungo FC ambao wametoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons, Nelson Mandela.

SOMA NA HII  HII HAPA, HADITHI YA YANGA NA MABAO 36 YA WAZALENDO....