Home Uncategorized KOCHA YANGA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MABAO MENGI

KOCHA YANGA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MABAO MENGI


ZLATKO Krmpotic, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanajukumu kubwa moja la kufanya kwenye mechi zao zote zilizobaki kufunga mabao mengi yatakayowapa nafasi ya kuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi zinazokuja.


Kwa sasa Yanga imecheza mechi tatu za ligi imefunga mabao matatu na kufungwa bao moja huku kibindoni ikiwa na pointi saba baada ya kukamilisha raundi ya tatu nafasi yake ni ya tano.

Ilianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons kisha ikaambulia ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

Raia huyo wa Serbia amesema:”Kikubwa tunahitaji ushindi kwenye mechi zetu hilo ni jambo la kwanza pia kwa kuwa tumekuwa na tatizo la kufunga mabao mengi jukumu lingine ni kuongeza umakini katika kutengeneza nafasi na kuzimalizia pia.

“Kwa kufanya hivyo tutakuwa imara na kujiongezea hali ya kujiamini kwa wakati ujao muhimu kuwa na ushindi na kufunga mabao mengi.”

Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 27, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mabao ya Yanga yamepachikiwa kimiani na Lamine Moro ilikuwa mbele ya Mbeya City, Michael Sarpong mbele ya Tanzania Prisons na Mukoko Tonombe mbele ya Kagera Sugar.
SOMA NA HII  SABABU ZA MAKOCHA MBAO FC KUBWAGA MANYANGA HII HAPA