Home Uncategorized MASHINE HII HAPA YA KAZI NDANI YA SIMBA KUIBUKIA TAIFA LEO, NI...

MASHINE HII HAPA YA KAZI NDANI YA SIMBA KUIBUKIA TAIFA LEO, NI FUNDI WA KUPIGA MASHUTI YA MBALI


JONAS Mkude, kiungo mkabaji wa Simba leo yupo fiti kuvaana na Azam FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

Mchezo huu wa leo ni wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo mshindi atakayepenya jumla hatua ya nusu fainali atakutana na Yanga ambao walishinda jana, Juni 30 kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Kagera Sugar mabao 2-1.

Mkude alikuwa nje akitibu majeraha yake ya kidole cha mguu wa kulia alichoumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, Juni 8, Uwanja wa Mo Simba Arena.

Mchezo huo Simba ilishinda mabao 3-1 na mabao yalifungwa na John Bocco aliyetupia mawili na Ibrahim Ajibu alitupia moja huku kwa upande wa KMC likipachikwa kimiani na Charles Ilanfya.

Mkude licha ya kuwa nje akitibu majeraha pia alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa kitendo cha kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United Uwanja wa Taifa adhabu hiyo tayari imekamilika.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa anaamini kwamba wachezaji wake wote wapo tayari kupambana kupata matokeo.

Mkude ana uwezo mkubwa kwenye kupiga mashuti ya mbali na anaweza kufunga na kutengeneza nafasi za mabao.

Simba ikiwa imefunga mabao 69 ametupia mabao mawili na kutengeneza pasi mbili za mabao.

SOMA NA HII  WATANZANIA WATATU WATWAA UBINGWA HUKO CONGO