Home Uncategorized WATANZANIA WATATU WATWAA UBINGWA HUKO CONGO

WATANZANIA WATATU WATWAA UBINGWA HUKO CONGO


NYOTA watatu kutoka ardhi ya Bongo ambao ni Thomas Ulimwengu, Ramadhani Singano na Eliud Ambokile ni miongoni mwa waliobeba ubingwa na TP Mazembe baada ya timu hiyo kutangazwa Bingwa wa Ligi Kuu ya DR Congo maarufu kama Lina foot.

 TP Mazembe imetangazwa kuwa bingwa kutokana na Shirikisho la Soka DRC kuamua kumaliza Ligi zikiwa zimebaki mechi 7 kwa kila timu kutokana na hofu ya Corona.

Ambokile amesema kuwa kutokana na janga la Corona hakukuwa na shughuli ya kimechezo ambayo ilikuwa inaendelea hata mazoezi walikuwa wanafanya ndani.

“Hakukuwa na jambo la michezo ambalo linaendelea kutokana na janga la Corona hata mazoezi tunafanyia ndani kwani Serikali imezuia mikusanyiko isiyo ya lazima,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI