Home Uncategorized BUKAYO SAKA AONGEZA DILI REFU NDANI YA ARSENAL

BUKAYO SAKA AONGEZA DILI REFU NDANI YA ARSENAL


BUKAYO Saka, nyota wa timu ya Arsenal amesema kuwa anafurahi kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo kwa kuwa ni nyumbani na anapenda kuendelea kubaki hapo.

Ripoti zinaeleza kuwa Arsenal wamempa dili refu nyota huyo huku miaka aliyoongeza ikiwekwa kibindoni ili abaki ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo mwenye miaka 18 yupo tayari kuendelea kukipiga ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu Mikel Arteta.

Kabla ya kuongeza dili jipya nyota huyo alikuwa anawindwa na Liverpool, Manchester United pamoja na Bayern Munich.

Arteta amesema kila siku nyota huyo amekuwa bora kila wakati ndani ya Uwanja.

SOMA NA HII  BALAA LA MWILI JUMBA NDANI YA UWANJA LIPO HIVI