Home Habari za michezo MANARA ATUPA ‘JIWE LA GIZANI’ KUHUSU USAJILI WA AZIZ KI…KAMBI YA MAREKANI...

MANARA ATUPA ‘JIWE LA GIZANI’ KUHUSU USAJILI WA AZIZ KI…KAMBI YA MAREKANI NA UTURUKI ZAGEUKA NDOTO ZA MCHANA…


BAADA ya kufanikiwa kumsajili winga wa kimataifa raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, kikosi cha Yanga kinatarajia kuweka kambi yake Karatu, Arusha ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa watakayoshiriki.

Aziz Ki ambaye alikuwa akiichezea Asec Mimosas, alitambulishwa rasmi usiku wa kuamkia jana baada ya mabosi wa Yanga kukamilisha taratibu za usajili huo.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara alisema wale ambao walikuwa wanawabeza kuhusu kuipata saini ya nyota huyo sasa watakuwa wanaona vitendo.

“Kwa wale ambao walikuwa wanabeza kwamba hatuwezi kupata saini ya nyota mwenye uwezo mkubwa na namba 10 bora basi iwafikie kwamba tumempata na tupo naye ndani ya kikosi cha Yanga,”.

Wakati huo huo, taarifa zilizopatikana jijini jana zinasema Yanga itaenda kuweka kambi yake Karatu baada ya safari ya kwenda Uturuki kuota mbawa.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA NYONI KUTEMWA SIMBA....MBRAZILI KAMTAZAMA WEE...KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HILI..