Home Simba SC KOCHA GOMES, MWENDO WA PASI TATU BAO

KOCHA GOMES, MWENDO WA PASI TATU BAO


KOCHA wa Simba, Didier Gomes, ameonekana kuhitaji zaidi wachezaji wake watumie nafasi wanazozipata baada ya juzi kufanya zoezi la kugusa mpira mara chache na kufunga.

 

Simba wanakaribia kumaliza wiki sasa wakiwa nchini Morocco walikoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa.

 

Mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa madai ya kulinda weledi wa kazi yake aliliambia Championi Jumatatu kuwa kocha amekuwa akifanya mazoezi ya kumiliki mpira na kufunga na akiwataka wachezaji wasiguse mpira zaidi ya mara tatu.

 


“Kocha amekuwa akifanya mazoezi ya kumiliki zaidi mpira na kufunga mabao kwa haraka, hataki wachezaji wake waguse mpira zaidi ya mara tatu na kwa hakika hilo linafanyika kwa asilimia kubwa na wachezaji wamekuwa wakipatia sana,” alisema mtu huyo.

 

Gomes mwenyewe alinukuliwa akisema Morocco wanatakiwa kukamilisha program zote ambazo wamepanga kufanya: “Huku ni sehemu sahihi kwetu kutengeneza timu, kwa sababu msimu ujao utakuwa mgumu na ushindani mkubwa, hivyo inatakiwa tufanye kila kitu.”


Kwenye kambi hiyo ya Simba kuna nyota wapya ambao wamejiunga na timu hiyo ikiwa ni pamoja na Peter Banda, Israel Mwenda kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

SOMA NA HII  KUHUSU USHINDI WA SIMBA LEO DHIDI YA KAGERA....HAYA HAPA YA NYUMA YA PAZIA YAKUYAJUA...