Home Azam FC STAA MPYA WA AZAM ALIYESAJILIWA ‘JUU KWA JUU’ …AFUNGUKA MAMBO YALIVYO KWA...

STAA MPYA WA AZAM ALIYESAJILIWA ‘JUU KWA JUU’ …AFUNGUKA MAMBO YALIVYO KWA MABOSI HAO…KOCHA ATIA NENO…


Kiungo Mshambuliaji mpya wa Azam kutoka Muivory Coast, Tape Edinho amekiri kwa muda aliopo ndani ya timu hiyo, anaamini msimu ujao watatisha dhidi ya wapinzani.

Edinho alitua Azam hivi karibuni akitokea ES Bafinga ya Ivory Coast, alisema; “Nafurahi kuwa hapa, nimeshuhudia viwango vikubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu. Kila siku tunazidi kuzoeana na kucheza kwa maelewano makubwa na naamini hadi ligi inaanza tutakuwa na kikosi imara sana.”

“Nimesimuliwa kuhusu ligi hii, nachoweza kusema watu wasubiri msimu uanze kila mmoja ataona ubora wetu na tunajipanga kufanya mapinduzi makubwa kwenye soka la Tanzania.”

Kocha Mkuu wa Azam Abdihimid Moallin aliweka wazi kufurahishwa na viwango vya wachezaji wake wapya akiwemo Edinho huku akiamini msimu ujao watakuwa bora zaidi.

“Kila mchezaji anajaribu kuonesha kile alichonacho na kwa ujumla wako vizuri na msimu ujao utakuwa bora kama kila mmoja atajituma,” alisema Moallin.

Edinho ambaye inasemekana mabosi wa Azam walimvuta juu kwa juu akiwa njiani kwenda Ulaya, alikuwa mtamu msimu uliopita akichaguliwa kikosi bora na kuteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora.

SOMA NA HII  KISA UDHAIFU WA REAL BAMAKO...MAYELE AIONA ROBO FAINAL CAF...