Home Uncategorized HUYU HAPA NYOT WA AZAM FC AMEPEWA JUKUMU LA KUIMALIZA YANGA LEO

HUYU HAPA NYOT WA AZAM FC AMEPEWA JUKUMU LA KUIMALIZA YANGA LEO


NICHOLAUS Wadada, beki kisiki wa Azam FC leo amepewa kazi moja ya kuigoza safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa kuimaliza Yanga ya Mbelgiji, Luc Eymael.
Wadada amekuwa ni injini ndani ya Azam FC kwa kuhusika kwenye jumla ya mabao matano kati ya 20 ambayo wamefunga Azam na ameongoza safu yake ya ulinzi kuruhusu mabao nane ya kufungwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji wote wamepewa majukumu ya kufanya ndani ya Uwanja ili kuipa timu matokeo mbele ya Yanga ikiwa ni pamoja na Wadada.
“Wachezaji wote wamepewa majukumu ya kufanya haimaanishi Wadada pekee ndiye amepewa kila mchezaji ana kazi yake ndio maana unaona timu inapata matokeo kwa kuwa wanacheza kwa kushirikiana.
“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi tunapambana kuona namna gani tutafikia malengo ambayo tumejiwekea ndani ya ligi pamoja na Shirikisho kwani kila mechi ina mtindo wake wa kipekee,” amesema Cheche.
SOMA NA HII  NYOTA HAWA WATATU WA YANGA, MMOJA AMEACHWA MAZIMA,WAWILI MAMBO HAYAELEWEKI