Home Habari za michezo AJIBU: – SIKUZALIWA SIMBA NA YANGA…KWANZA MIMI MWENYEWE NIMEWAKATIA TAMAA…

AJIBU: – SIKUZALIWA SIMBA NA YANGA…KWANZA MIMI MWENYEWE NIMEWAKATIA TAMAA…

Ajibu akiwa Singida Big Stars

Kiungo Mshambuliaji wa Kikosi cha Singida Big Stars, Ibrahim Ajibu Migomba amewashukia mashabiki ambao wamekuwa wakidai kuwa amechelewa kwenda kucheza soka la kulipwa Barani Ulaya mpaka kiwango chake kimeporomoka.

Ajibu amesema wakati akihojiwa mara baada ya timu yake kuahindwa kuchukua Kombe la Mapinduzi Zanzibar kufuatia kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Mlandege FC ya Zanzibar juzi Ijumaq, Januari 13, 2023, usiku.

“Mimi kuondoka katika vilabu hivyo wala hakujanivunja moyo kwa sababu mimi sijazaliwa Simba, Yanga wala Azam mimi nimezaliwa mtaani kwangu, kwa hiyo sehemu zote hizo mimi napita tu kama kazi mpaka safari yangu ya mpira itakapoisha.

“Kama kuna mtu amenikatia tamaa kwenye kipqji changu cha mpira hata mimi pia nimemkatia tamaa vilevile.

“Maneno wanayosema mashabiki mtandaoni hayaniumizi kichwa kwa sababu siwasikii. Kwanza mimi mambo ya mtandaoni siyafuatilii sijui Instagram mini, mimi sio mchongo wangu kabisa, kwa hiyo mtu akinitumia matusi Instagram ni kama vile anamtumia mbuzi, sasa ushaona mbuzi anajua kusoma?

“Wanaolalamika siendi kucheza Ulaya hata shabiki pia ana opportunity ya kwenda Ulaya kwenye biashara zake na shughuli zake anazofanya kama anaona kwenda Ulaya ni rahisi na yeye ajitahidi aende Ulaya.

“Usimwambie mtu kwenda Ulaya kwa sababu unamuona kwenye shughuli yake ukadhani ni rahisi Kwa sababu hii mimi ni kazi yangu unajua mtu mwingine anadhani mimi naenjoy tu kwenye mpira wakati hii ndio shughuli yangu. Kwa hiyo kama mtu anaona kwenda Ulaya ni rahisi na yeye katika shughuli zake ajitahidi aende Ulaya.

“Wanaochukua mkaa Ulaya pia watu wanapikia mkaa ajitahidi kwenda kupeleka mkaa wake Ulaya akauze kama ni rahisi,” Maneno ya Mchezaji Ibrahim akihojiwa na waandishi wa habari.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA RIVERS UNITED, UWANJA WA MKAPA