Home Habari za michezo DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA DODOMA…SURE BOY LAMKUTA JAMBO YANGA…KAZE AJIPIGA...

DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA DODOMA…SURE BOY LAMKUTA JAMBO YANGA…KAZE AJIPIGA KIFUA…


CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga, amesema wachezaji wote ambao walikuwa hawapo fiti kutokana na sababu mbalimbali, wameshaanza mazoezi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, hivyo wapinzani wao watakutana na busta la maana.

Ni Khalid Aucho na Kibwana Shomari, hawa walipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Prisons, lakini waliendelea kucheza, huku kipa Djigui Diarra akikwama kuyeyusha dakika 90.

Kaze amesema kwenye mazoezi ya mwisho, wachezaji hao walifanya vizuri na wenzao hali iliyoonesha wapo vizuri, lakini kiungo Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ akiendelea kukosekana.

“Aucho na Kibwana tayari wameanza mazoezi kwa kuwa mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons walipata maumivu, lakini waliendelea na mchezo mpaka wakakamilisha dakika 90.

“Sure Boy yeye bado anaumwa malaria na hajaanza mazoezi na wenzake, lakini anaendelea vizuri, hivyo kwa mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji tunaamini tutakuwa kamili kusaka pointi tatu,” alisema Kaze.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema: “Ushindi ndio jambo pekee ambalo litatufanya kurejea katika furaha, tumeshindwa kupata ushindi michezo iliyopita jambo ambalo tunahitaji kurekebisha kupitia mchezo huu.”

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 57 baada ya kucheza mechi 23, katika mechi tatu zilizopita za ligi hiyo, haijashinda. Leo itacheza dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

SOMA NA HII  YANGA WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWENYE DILI LA MANZOKI...NABI AINGILIA MCHEZO NA KUHARIBU MAMBO USIKU USIKU...