Home Habari za michezo KUHUSU SIMBA KUMSAJILI MAYELE….AHMED ALLY KAIBUKA NA JIPYA HILI…AGUSIA KUSEPA KWA BALEKE..

KUHUSU SIMBA KUMSAJILI MAYELE….AHMED ALLY KAIBUKA NA JIPYA HILI…AGUSIA KUSEPA KWA BALEKE..

Habari ya Simba SC

Baada ya taarifa kusambaa za kuondoka kwa Mshambualiaji kinara wa Simba SC, Jean Baleke huku ikisemekana ameachana na Timu hiyo, Meneja wa Habari wa Simba SC Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Naona mnafurahia taarifa za kuondoka Baleke

Niwataarifu tuu Baleke atarejea hivi punde baada ya kupata hati mpya ya kusafiria ( Passport) na atajiunga na timu Uturuki kwa Pre Season

Lakini niwaambie tuu kama tukiamua kumuondoa Baleke nyie ndio mtaathirika zaidi maana tutachukua uyo Mkongo mwenzie aje kuziba nafasi

Sasa jukumu lenu ni kumuombea dua Baleke apate Passport yake mapema arudi kazini”

Hata hivyo jana Baleke alirudi nchini na mapema hii leo mchana alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba waliokwea pipa kuelekea nchini Uturuki kuweka kambi ya wiki tatu.

Taarifa za kutoka ndani ya Simba zinadai kuwa Baleke ameamua kuendelea kukipiga na wekundu hao wa msimbazi mara baada ya kuridhishwa na hali ya kuaminiwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Robartinho.

Itakumbukwa kuwa Baleke alitua nchini na kujiunga na Simba , kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January ambapo toka amejiunga na timu hiyo amekuwa na moto wa kuotea mbali katika kuzifumania nyazu za timu pinzani.

Baleke awali alikuwa TP Mazembe ambapo kutokana na ukubwa wa kikosi cha timu hiyo alitolewa kwa mkopo kwenye moja ya timu za Asia kabla ya Simba kumchukua kwa mkopo wenye kipengelea cha kusalia moja kwa moja endapo atafanya vyema.

SOMA NA HII  SHEVA HATIHATI KUACHWA SIMBA