Home Uncategorized LIPULI YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA AZAM FC SAMORA,IRINGA

LIPULI YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA AZAM FC SAMORA,IRINGA


PAUL Materazi nyota wa Lipuli FC ya Iringa alitibua mipango ya Azam FC kusepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo, Julai 19 Uwanja wa Samora. 

Bao lake la dakika ya 80 lilifanya ubao wa Uwanja wa Samora usomeke 1-1 kwani Azam FC walianza kupachika bao la kwanza kupita kwa Abdallah Heri dakika ya 44.

Sare hiyo inazidi kuyadumaza matumaini ya Azam FC kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwani wameachwa na wapinzani wao Yanga kwa jumla ya pointi mbili.

Yanga kibindoni ina pointi 68 huku Azam FC ikiwa na pointi 66 zote zimecheza mechi 36 zimebakiwa na mechi mbili mkononi.

Sare hiyo pia ni furaha kwa Lipuli kwani inazidi kujinasua kwenye hatari ya kushuka jumlajumla kwa kukaa kwenye mstari mwingine wa kundi la kucheza playoff.

Ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 41baada ya kucheza mechi 36 imebakiwa na mechi mbili kumaliza mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  PIALALI ALIYEMKALISHA TINAMPAY, MTANGO WATOA NENO LA SHUKRANI