Home Uncategorized PIALALI ALIYEMKALISHA TINAMPAY, MTANGO WATOA NENO LA SHUKRANI

PIALALI ALIYEMKALISHA TINAMPAY, MTANGO WATOA NENO LA SHUKRANI


 MABONDIA wa ngumi za kulipwa waliokuwa na mapambano ya kimataifa Novemba 28, mwaka huu, Idd Pialali na Salim Mtango, leo Desemba Mosi wametembelea ofisi za kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Championi,  Spoti Xtra, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi kwa ajili ya kutoa shukrani kutokana na sapoti kubwa waliyoipata katika kufanikisha mapambano yao.

 

Mabondia hao wote wawili walishinda kwa pointi mapambano yao yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Next Door Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo, Pialali alimshinda Mfilipino, Arnel Tinampay, huku Mtango akishinda dhidi ya Eduardo Mancito.


Bondia mzawa Pialali amesema: “Napenda kuwashukuru wale wote waliofanya kazi kubwa ya kufanikisha pambano dhidi ya Tinampay.

 

“Kwa namna ya pekee namshukuru Promota Kapteni Selemani Semunyu na kampuni ya Global Publishers kwa mchango mkubwa mpaka kufanikisha mapambano hayo.”


Kwa upande wake, Mtango amesema: “Tunawashukuru wadau wote waliopambana kufanikisha mapambano yetu, hatuwezi kuwataja mmojammoja lakini ni wazi walifanya kazi kubwa,”

 

Mabondia wengine walioambata nao ni, Selemani Kidunda, Ismail Galiatano na  Adam Kipenga.

 

 

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUMCHAKAZA WILDER KWA TKO, FURRY ALIKUWA AMEONGOZA RAUNDI ZOTE SABA KWA POINTI