Home Simba SC KUUZWA KWA CHAMA NA LUIS KWAWASHTUA WAARABU..HIVI NDIVYO MEDIA ZA HUKO...

KUUZWA KWA CHAMA NA LUIS KWAWASHTUA WAARABU..HIVI NDIVYO MEDIA ZA HUKO ZINAVYOANDIKA


ISHU ya Simba kuwauza mastaa wake wawili tegemeo, Luis Jose Miquissone na Clatous Chama imekuwa gumzo kwa wachambuzi wa Kiafrika hususani Kaskazini ambako wameonekana kushtushwa na uamuzi huo.

Lakini mitandao mingi imefichua kwamba biashara waliyoifanya Simba ni ya kiwango cha juu kwa klabu inayoanza kukua kibiashara.

Aidha, uamuzi wa Simba kupiga kambi mjini Rabat, Morocco nao umekuwa ukijadiliwa na vyombo vingi vya Kaskazini pamoja na Misri kwenyewe huku wakitabiri kwamba msimu huu huenda ikafanya makubwa zaidi ya robo-fainali.

Kundi la kwanza la Simba lilitua juzi Rabat, huku wengine wakitarajia kupaa jana akiwemo beki kitasa, Henock Inonga ‘Varane’ raia wa DR Congo aliyekuwa anakipiga DC Motema Pembe.

Awali, Varane alikuwa kwenye rada za Yanga kabla ya meneja wake kumpeleka Simba. Jana kamera zetu zimemnasa beki huyo mwenye rasta akiwa na wachezaji wengine wa Simba, Chris Mugalu, Ally Salim, Said Ndemla, Ibrahim Ajib, Yusuph Mhilu pamoja na mratibu wa timu hiyo Abas Suleiman kwenye Hospitali ya Muhimbili walipokwenda kupata chanjo ya Covid -19 tayari kwa safari.

Varane kama alivyopenda kuitwa, alifika hospitali hapo mishale ya saa 7:00, akiwa amevaa pensi na tisheti za kijani iliyokolea sana, kofia nyeusi na raba kali iliyochanganya rangi akiongozana na Mkongomani mwenzake Mugalu sambamba na Abas, Mhilu na Ally na kulekea katika kitengo cha Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) ambapo chanjo ya Covid -19 inatolewa.

Baada ya kufika kwenye jengo hilo ghorofa ya nne, waliendelea na taratibu zote za kupatiwa chanjo ikiwemo kupewa elimu ya chanjo na dakika chache Ndemla na Ajibu walifika na wote kuchanjwa kwa pamoja. Ndemla na Ajibu walikuwa watemwe Simba lakini wakanusurika dakika za mwisho juzi mchana.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE: NILISHANGAA SIMBA WALIPOMSAJILI KISUBI...AFUNGUKA ISHU YA NKANE NA YANGA...