Home Habari za michezo AHMED ALLY:- JAHAZI LA SIMBA LINAYUMBA….TUTAPUNGUZA WACHEZAJI MIZIGO KWA TIMU…

AHMED ALLY:- JAHAZI LA SIMBA LINAYUMBA….TUTAPUNGUZA WACHEZAJI MIZIGO KWA TIMU…

Habari za Simba leo

Meneja Habari na Mawasilino Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri msimu huu, wanatarajia kupunguza baadhi ya wachezaji ambao wameonekana kutoisaidia timu hiyo.

Ahmed ametumia kauli ya kisanaa kuwa kama jahazi linazama basi upo umhimu wa kupunguza mizigo kwenye jahazi hilo ili lisizame kabisa.

“Nadhani kwa sasa Wanasimba tunapaswa tushirikiane ili tumalize ligi salama na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu ujao.

“Baada ya hapo tutakwenda kukaa chini sisi kama viongozi wa Simba SC na kuangalia nini tufanye, wapi turekebishe, lakini kwa kuwa timu yetu msimu huu haijafanya vizuri, maana yake tuna wajibu wa kufanya maboresho makubwa ili tuwe na msimu ujao mzuri.

“Kama jahazi linayumba, kuna mambo mawili, kwanza kupunguza mizigo ili likae sawa, au ugeuze, urudi pwani ili ujipange upya, kwa hiyo sisi kuna mambo tutayafanya ili kujiweka vizuri, sisi kama viongozi tunajua nini cha kufanya kuelekea msimu ujao,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI WOTE A-Z KUHUSU MAYELE KUVUNJA MKATABA MISRI....SIMBA WATAJWA...