Home Habari za michezo TETESI:- JOBE, FREDDY KUPEWA ‘THANK YOU’ SIMBA…MASTAA WENGINE HAWA HAPA…

TETESI:- JOBE, FREDDY KUPEWA ‘THANK YOU’ SIMBA…MASTAA WENGINE HAWA HAPA…

Habari za Simba leo

Washambuliaji wa Simba Sc, Pa Omar Jobe na Freddy Koubalan huenda huu ndiyo ukawa msimu wao wa kwanza na wa mwisho kuonekana katika Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na moja ya mashart ya mkabata wao waliosaini na klabu ya Simba ni kuonyesha kiwango bora na cha kuisaidia timu kwa nyakati zote.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakikupenda kutwaja jina; kimesema wachezaji hao walipewa mkabata wa miezi sita wenye kipengele cha iwapo wakifanya vizuri wataongezewa mkabata.

Nyota hao waliosajiliwa kwa pamoja kwenye dirisha dogo la msimu uliopita wakichukua nafasi ya Moses Phiri na Jean Othos Baleke, wameshindwa kuonesha ubora na kuisaidia timu hiyo pakubwa kama ambavyo yalikuwa matarajio ya Wanamsimbazi.

Tayari maneno ni mengi kutoka kwa mashabiki na wanachama wa Simba na hata viongozi wa zamani na wa sasa wa Simba wakiponda usajili wa wachezaji hao kuwa hauna tija wala haujawa na matunda kwenye kuchagiza malengo na mafanikio ya klabu.

Hata hivyo, Freddy anaweza kuponyeka kwenye panga hilo kutokana na kuanza kuonyesha uwezo wa kufunga magoli tofauti na Jobe ambaye anawakati mgumu ndani ya kikosi hiko cha Benchikha.

Jana kwenye mchezo wa watani wa jadi, Freddy aliifungia Simba goli la kufutia machozi wakati alipoingia kuchukua nafasi ya Ntibazonkiza.

SOMA NA HII  YANGA HII YA GAMONDI NI ZAIDI YA BALAA NA NUSU...MAAJABU YAKE YAWATESA SIMBA USIKU NA MCHANA...