Home Habari za michezo ALLY KAMWE:- TUNA OFA KWA AZIZI KI KUTOKA AFRIKA KUSINI, MOROCCO NA...

ALLY KAMWE:- TUNA OFA KWA AZIZI KI KUTOKA AFRIKA KUSINI, MOROCCO NA MISRI….

Habari za Yanga leo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema mpaka sasa klabu hiyo imeshapokea ofa za wachezaji watano kutakiwa na klabu mbalimbali za barani Afrika na Asia, ikiwemo uhitaji wa Aziz Ki.

Akizungumza na HabariLEO, Kamwe amesema Aziz Ki ofa zake zimekuwa zikijirudia “Mtu kama Aziz ofa zake zinajirudiarudia tu, leo utakisikia kutoka South Afrika, kesho Morocco, kesho ofa Misri zinajirudia tu.”

Kamwe amesema baada ya ofa hizo kinachofuata ni kuzijadili kwenye uongozi kuona kama kuna uwezekano wa kuruhusiwa au kubaki nao, amesema wameshazungumza na baadhi ya wachezaji mambo yanaenda vizuri.

Pia Kamwe amegusia tetesi za Mzize kutakiwa na Azam FC, ambapo hakuthibitisha ila amesema alizungumza na Mzize na kumpa mawili matatu. –

Hata hivyo Mzize inafahamika kuwa kashasaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Yanga kwa muda wa miaka 2 zaidi.

SOMA NA HII  BOSI WA YANGA ASEMA HAYA KWA WALIWACHUKULIA POA KUWEKA KAMBI NCHINI