Home Uncategorized YANGA KUREJEA MAZOEZINI RASMI JUNI MOSI

YANGA KUREJEA MAZOEZINI RASMI JUNI MOSI

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa timu yao itaanza mazoezi Juni mosi baada ya Serikali kuruhusu shughuli za Michezo kuanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, Mei 21 alitangaza kuzirejesha shughuli zote za michezo ambazo zilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Ofisa Habari Yanga, Hassan Bumbuli amesema:- “Sisi tutaanza mazoezi rasmi Juni Mosi na tayari tumewasiliana na wachezaji kuhakikisha wanakuwepo karibu na Dar es Salaam kabla ya muda huo kufika,” amesema.

SOMA NA HII  BAKARI SHIME AAHIDI FURAHA KILIMANJARO QUEENS