Home Uncategorized BOXER APEWA SOMO NA NAHODHA WA YANGA

BOXER APEWA SOMO NA NAHODHA WA YANGA

PAUL Godfrey maarufu kama Boxer amepewa somo na nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Abdul kuwa anapaswa kuongeza juhudi ili kufikia malengo aliyojiwekea.

Boxer alikuwa chaguo la kwanza msimu wa 2018/19 chini ya Kocha Mkuu,  Mwinyi Zahera ila kwa sasa hajawa chaguo la kwanza mbele ya Luc Eymael. 

Akizungumza na Saleh Jembe,  Abdul amesema kuwa Boxer ana uwezo mkubwa akiwa ndani ya uwanja ila ni lazima aongeze juhudi kufikia malengo aliyojiwekea. 

“Anafanya vizuri na juhudi anazo pia ila lazima aongeze juhudi zaidi na zaidi kufikia yale aliyojiwekea kwani bado ana muda wa kufanya makubwa,” amesema. 

Boxer ana bao moja kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara ambalo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Singida United wakati waliposhinda mabao 3-1 Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  NYOTA MPYA WA YANGA, RAIA WA RWANDA SIBOMANA AAMUA KUFANYA KWELI, AMSHUSHA MKEWE DAR