Home Habari za michezo SIMBA SC WAINGIA MCHECHETO NA NGUVU ZA YANGA…AHMED ALLY AFICHUA JAMBO HILI…

SIMBA SC WAINGIA MCHECHETO NA NGUVU ZA YANGA…AHMED ALLY AFICHUA JAMBO HILI…

Ahmed Ally Simba SC

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kitendo cha Azam FC kupoteza dhidi ya Young Africans kimewaongezea hofu ya kuuwania Ubingwa msimu huu 2022/23.

Azam FC ilipoteza dhidi ya Young Africans Jumapili (Desemba 25) kwa kufungwa 3-2, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na kuifanya Ligi Kuu kuendelea kuwa na upinzani mkali kwenye nafasi ya kuwania Ubingwa huku Wananchi wakipewa kipaumbe la kutetea Taji.

Ahmed Ally amesema waliamini Azam FC wangeweza kuisimamisha Young Africans katika mchezo huo ili kupunguza makali ya kuufukuzia ubingwa, lakini imekuwa tofauti na sasa hawana budi kuhakikisha wanashinda michezo iliyosalia.

“Tukisema haitutii hofu tutakuwa wanafiki ukweli ni kwamba, inatutia hofu. Hofu imeongezeka zaidi baada ya mpinzani wetu kushinda dhidi ya Azam FC.”

“Azam FC tulieahesabu kama timu inayopigania ubingwa msimu huu, kwa hiyo tulitarajia pengine wangeweza kumpunguza kasi yule ambaye tuponae kwneye mbio za ubingwa.”

“Kitendo cha Azam kupoteza kimempa faida mpinzani wetu tunaeshindananae kwenye mbio za ubingwa. Imetushtua na kutufanya tuwe makini zaidi na kazi zaidi inabidi kufanywa.”

“Kazi tuliyonayo kwa sasa sio kushinda tu mechi zetu lakini pia inabidi mpinzani wetu apotee ili tuweze kupunguza gape la alama.”

“Gape linashtua lakini halipaswi kutuondolea umakini wetu, tuendelee kupambana na kupigania alama tatu.” amesema Ahmed Ally

Young Africans inaongoza Msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 47, ikiizidi Simba SC kwa tofauti ya alama 6, baada ya Timu hiyo ya Msimbazi kuipasua KMC FC juzi Jumatatu (Desemba 26), mabao 3-1, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Azam FC imebaki nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 37, baada ya kucheza michezo 18.

SOMA NA HII  PATRICK AUSSEMS AKIMBIA TIMU KENYA....AISHIA KUWAPA MATUMAINI KWA 'VIDEO CALL'...TIMU YA RWANDA YATAJWA KUHUSIKA...