Home Yanga SC MZEE MPILI: SIMBA LAZIMA WAFUNGWE KIGOMA

MZEE MPILI: SIMBA LAZIMA WAFUNGWE KIGOMA


 HAJI Omari maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa hakuna namna ambayo wapinzani wao Simba wanaweza kufanya kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho, lazima wafungwe.

Simba inakwenda kukutana na Yanga, Julai 25 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho ikiwa na kumbukumbu ya kunyooshwa kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa Julai 25.

Kabla ya mchezo huo uliokuwa na sarakasi nyingi, Mzee Mpili aliibuka na kuweka wazi kwamba Yanga itashinda bao moja na baada ya dk 90 ngoma ilisoma Simba 0-1 Yanga.

Mzeee Mpili kuekelea mchezo huo amesema:”Mimi nina watu na tunacheza mpira kwa hesabu kubwa ili kuona kwamba tunashinda. Kuelekea kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba, kweli Kigoma hawatoki.

“Ndani ya dakika 90 za mchezo hapo tayari mpira umekwishwa na tumepata kabisa ushindi kwani sisi tunahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho.

“Nimeona kwamba na Simba nao wanatamba kwamba wanahitaji kushinda basi subiri na tuone hao wote wanaozungumza tutakutana nao Kigoma,” amesema.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA SIMBA KESHO....'SURE BOY' AOMBA MSAADA WA MASHABIKI ...HASIRA ZA KIPIGO CHA VIPERS ZAMTIA 'WAZIMU'...