Home Habar za Usajili Simba KUHUSU USAJILI ….SIMBA WAANIKA MPANGO WA KUVUTA MASTAA WAKUBWA ZAIDI…” USAJILI HAUJAISHA...

KUHUSU USAJILI ….SIMBA WAANIKA MPANGO WA KUVUTA MASTAA WAKUBWA ZAIDI…” USAJILI HAUJAISHA BADO”….


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema Klabu yao haijafunga usajili wake kwani bado inapambana kusaka wachezaji wengine kuimarisha kikosi ili kuhakikisha wanafikia malengo yao msimu ujao.

“Tunaomba radhi kwa msimu uliopita lakini ilikuwa ni funzo. Tunafanya kazi kuhakikisha tunafanya usajili mzuri ili tusisimamishwe na mtu yeyote. Tumejipanga kuwa na msimu bora zaidi.

“Kwanza niseme Simba usajili hatujamaliza. Sasa taarifa rasmi kuhusu usajili wa Simba nenda kwenye platforms za Simba. Najua CEO wiki hii ataachia kitu. Nawahakikishia tupo vizuri na tutaendelea kuwa vizuri,” amesema Mangungu.

SOMA NA HII  MWALIKO WA WASUDAN WAMFANYA MAKI KUFUNGUKA YA MOYONI...ATAJA MASTAA WALIOPO TIMU YA TAIFA...