Home Habari za michezo KIWANGO CHA NUNEZ CHAMTIA WAZIMU KLOPP…ASHINDWA KUJIZUIA AWATUPIA DONGO WALIOMSEMA VIBAYA…

KIWANGO CHA NUNEZ CHAMTIA WAZIMU KLOPP…ASHINDWA KUJIZUIA AWATUPIA DONGO WALIOMSEMA VIBAYA…


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemwagia misifa, straika wake mpya Darwin Nunez, baada ya kukiwasha kwenye mechi yake ya kwanza, dhidi ya Manchester city akiwa na uzi huo akitokea Benfica.

Nunez alifunga bao la kwanza kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, dhidi ya Man City na kusababisha penalti iliyozaa bao.

Awali taarifa zimeripoti Nunez anahitaji muda wa kuzoea mfumo anaotumia Klopp, lakini wikiendi iliyopita straika huyo alidhihirisha kuwa ni mtamabo wa mabao baada ya kuipa Liverpool ushindi.

Nunez alijiunga na Liverpool kwa kitita cha Pauni 64 milioni akitokea Benfica, lakini mkwanja huo utaongeza kufikia hadi Pauni 75 milioni. Na endapo kiwango chake kitaimarika  kuna uwezekano wa pesa hiyo ikaongeza zaidi.

Akizungumza baada ya mechi iyo Klopp amesema Nune alionyesha kiwango kizuri na kupagawisha mashabiki wa Liverpool, waliyofurika kwenye uwanja King Power.

“Nunez alikuwa vizui mno, nilisema atakuwa sawa tu, watu wanapenda kutoa hukumu mapema, hii ni mechi yake kwanza, hii haimjengi mchezaji kabisa, lakini mambo kama haya yanatokea kwenye soka,” alisema Klopp.

“Timu zote hazikuwa fiti asilimia 110, hata sisi kuna wakati mechi ilikuwa ngumu kwa upande wetu, kila mtu alipaniki, lakini muhimu tuna subira na tutafanya mambo mazuri,” aliongeza.

Liverpool ilibeba Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza tangu miaka 16 iliyopita ilipochukua.

SOMA NA HII  UKIONA YANGA WANACHEZA JUMANNE TU...NENDA KABET WANAFUNGWA...TAKWIMU HIZI HAPA...