Home Habari za michezo YULE STARIKA KUTOKA UGANDA ANAYELILIA KUSAJILIWA SIMBA….SAFARI HII KAJA NA HILI JIPYA…AENDELEA...

YULE STARIKA KUTOKA UGANDA ANAYELILIA KUSAJILIWA SIMBA….SAFARI HII KAJA NA HILI JIPYA…AENDELEA ‘KUIKAUSHIA’ KLABU YAKE…


Mshambuliaji wa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Cesar Manzoki amesema ana nafasi finyu ya kuendelea kuwatumikia Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC.

Mshambuliaji huyo ambaye ni Mzaliwa wa DR Congo ametoa kauli hiyo kufuatia mkataba wake na klabu ya Vipers kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu 2021/22, huku akitoa mchango mkubwa wa kuiwezesha kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Uganda.

Manzoki amesema wakala wake amemwambia kuna ofa nyingi zimetumwa sambamba na ile ya Vipers FC ambayo inapigania kumbakisha, hivyo kwa sasa anajitayarisha kutangaza wapi atakapocheza msimu ujao.

“Kuna asilimia ndogo za mimi kusalia hapa na kuna asilimia kubwa za kuondoka, kuna ofa ninazo ikiwemo ile ya kusalia niliyopewa na uongozi wa timu, pia ofa nyingine ikiwemo ya Simba.”

“Hivyo ndani ya siku chache zijazo nadhani nitakuwa nimekamilisha mchakato mwingine ambao utaenda kubadilisha historia yangu katika mpira.”

“Ni jambo la subira kwa kuwa ni mambo ya usajili, hivyo huhitaji mpaka mchakato ukamilike ndiyo kujadiliwa, lakini itakuwa mbaya kama tutazungumza jambo halafu dili likashindwa kutimia,” amesema Mshambuliaji huyo anayewaniwa na Simba SC ya Tanzania.

SOMA NA HII  AZAM FC WAMPA DILI LA MWAKA MMOJA BEKI MCAMEROON