Home Habari za michezo URAIS YANGA….INJINIA HERSI ADHAMIRIA AISEE…MWAKALEBELA AMGEUKA DK MSOLA DAKIKA ZA JIONI…AJITOA…

URAIS YANGA….INJINIA HERSI ADHAMIRIA AISEE…MWAKALEBELA AMGEUKA DK MSOLA DAKIKA ZA JIONI…AJITOA…


WAKATI jana Juni 9,2021 ikiwa ni siku ya mwisho ya kurejesha fomu na leo mchujo kuweza kuanza jana Injinia Hersi Said amerejesha fomu yake ya kugombea Urais wa Yanga.

Injinia amewakilishwa na wazee wa Yanga pamoja na Fredrick Mwakalebela ambaye rasmi amesema kuwa yeye hatogombea na kuwaaga wana Yanga kwenye nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi juzi alichukuliwa fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Julai na wazee wa klabu hiyo.

Jana wazee wa Klabu ya Yanga wamerudisha fomu hiyo ikiwa imejazwa tayari kwa kuanza mbio za Urais wa Klabu hiyo.

Mwakalebela amesema kuwa Yanga wanatambua namna Injinia alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  KOCHA COASTOAL UNION ASALENDA KWA YANGA..."WALITAKIWA KUTWAA UBINGWA AFRIKA