Home Uncategorized NIDHAMU YAIBEBA ARSENAL IKIICHAPA DUNDALK 3-0

NIDHAMU YAIBEBA ARSENAL IKIICHAPA DUNDALK 3-0


MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa wachezaji wake wameweza kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dundalk kwa sababu walicheza kwa nidhamu. 

Mchezo huo wa Europa League uliochezwa Uwanja wa Emirates umeifanya Arsenal kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kufikisha pointi 6 na imefunga jumla ya mabao 5 baada ya kucheza mechi 2 huku Dundalk ikiwa nafasi ya nne na haina pointi kwa kuwa imepoteza mechi zote mbili.

Arteta alishuhudia kijana wake Eddie Nketiah dakika ya 42 akipachika bao la kwanza zikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya mapumziko huku lile la pili lilipachikwa na Joe Willock dk ya 44 na la tatu dk ya 46 na Nicolas Pepe mabao ambayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo. 

Arteta amesema kuwa walicheza kwa nidhamu kubwa jambo ambalo limewapa ushindi wana imani ya kupambana kwa ajili ya mechi zao zijazo ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Manchester United ambayo ni ya Ligi Kuu England itakayochezwa Novemba Mosi.

SOMA NA HII  MOLINGA APANIA KUFUNGA MABAO MENGI KWENYE LIKI