Home Habari za michezo KUTOKA KUWA MKIMBIZI MPAKA KUSAJILIWA SIMBA SC….HAYA NDIO MAPITIO HALISI YA KIBU...

KUTOKA KUWA MKIMBIZI MPAKA KUSAJILIWA SIMBA SC….HAYA NDIO MAPITIO HALISI YA KIBU DENIS…

Habari za Simba SC

Upo msemo mmoja wa Kiingereza unasema ‘Trust the process’ kwa maana ya kuamini katika mchakato, huku ukitarajia matokeo chanya, msemo ambao kwa sasa unaendana kwa ukaribu na maisha ya mchezaji wa Simba SC, Kibu Denis Prosper.

Kutoka moja ya kambi za wakimbizi mkoani Kigoma alikolelewa, Kibu ndoto yake kuu ilikuwa ni kucheza soka katika viwango vya juu na akaamini katika mchakato wake ambao ni kucheza kwa juhudi na kufuata misingi ya soka ilivyo bila kujali nini na nani anasema nini.

Alicheza timu kadhaa Kigoma katika ngazi za chini akiamini katika mchakato na baadae akafunga safari hadi Mkoani Kagera na kujiunga na klabu ya Kumuyange FC iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la pili wakati huo ikitafuta kupanda Ligi Daraja la Kwanza lakini kwa sasa iliuzwa Dodoma na inaitwa Fountain Gate iko Championship.

Kibu Denis | Simba SCTimu hiyo iliyokuwa na masikani yake mitaa ya Kumuyange na Kumunazi wilayani Ngara ilimuamini Kibu na kuwa moja ya mastaa wake na yeye akaamini katika mchakato akakiwasha na mwisho wa siku kuonekana na Geita Gold kipindi hicho ikiwa Daraja la Kwanza na kumsajili.

Pale Geita alicheza kwa msimu mmoja kwa kiwango cha hali ya juu akiamini katika mchakato na misingi ya soka huku ndoto yake ikiwa ni kucheza katika ngazi za juu na imani ikamlipa kwani alisajiliwa Mbeya City ya Ligi Kuu msimu uliofuata.

Kutoka Geita hadi Mbeya kujiunga na wababe wa jiji hilo, ilikuwa ni safari ya matumaini na furaha kwa Kibu kwani alifikisha ndoto yake ya kwanza kucheza Ligi Kuu na pili aliamini pale City ni sehemu sahihi kwake kufikia ndoto zake kubwa kubwa.

Kama ilivyokawaida yake kuishi katika imani ya mchakato, Kibu akiwa Mbeya City msimu wa 2020/2021 alicheza Ligi Kuu kwa kiwango bora na kuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi hicho.

Habari za SimbaUbora wake akiwa City ulizifanya timu za Simba SC, Yanga na Azam ambazo zinajinasibu kuwa vigogo wa ligi ya Bongo, kuanza kupigana vikumbo kutaka saini yake na mwisho wa siku Simba ikashinda na kumsaini kwa mkataba wa miaka miwili pia wakati akiwa City aliitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Msimu wa 2021/2022, Kibu alivaa uzi wa Mnyama kwa mara ya kwanza ikiwa ni miongoni mwa ndoto zake kubwa kucheza katika klabu kubwa nchini lakini hapo ndipo akajua kuwa bado anahitaji kuendelea kuamini katika mchakato.

Usajili wa Kibu kutua Simba uliibuka na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ilikuwa suala lake la uraia kwani hakuwa na uraia rasmi wa Tanzania na asili yake ikiwa ni DR Congo.

Hapo mengi yalisemwa na kutaka kumtoa mchezoni lakini alikaza nafsi na baadae kukamilisha taratibu zote na kupewa uraia wa Tanzania na ruksa sasa kuanza kukiwasha ndani ya Simba.

Saido Ntibazonkiza akisalimiana na Kibu Denis leo kwenye mazoezi ya Simba SC

Kibu baada ya hapo ni kama alikuwa na hasira na waliombeza na kumsema, alicheza msimu wake wa kwanza ndani ya Simba kwa mafanikio huku kila kocha aliyekuwa kikosini hapo akimtaja kama mchezaji mwenye nidhamu na mpambanaji zaidi.

Sifa hizo za makocha kwa Kibu, hazikuwazuia mashabiki wa soka nchini kuendelea kumbeza Kibu kwani kutokana na sababu wanazozijua wao waliamini Kibu sio mchezaji anayestahili kucheza Simba.

Mwamba hakukata tamaa na kama ulikuwa haujui, msimu huo 2021/2022, Kibu ndiye alikuwa kinara wa mabao ndani ya kikosi cha Simba kwenye ligi akiwa nayo nane na asisti nne namba ambazo washambuliaji wengine hawakuwa nazo.

Huku na kule msimu ukaisha na kuanza msimu huu na Kibu hali ikazidi kumweka ngumu ndani ya Simba lakini akaamini katika mchakato na kukaza buti.

Mwanzo wa msimu huu Simba ikasajili mastaa kibao tena wengine wanaocheza namba sawa naye, kina Agustine Okrah, Moses Phiri, Habib Kyombo, Dejan Georgijevic, huku wengine wakiwa Nelson Okwa, Victor Akpan, Nassoro Kapama na Mohamed Ouattara.

Wakati mastaa hao wapya wakitua Simba, mashabiki wengi wa chama hilo walitaka Kibu aondoke hata kwa mkopo wakiamini sio saizi yao, lakini uongozi ukambakiza na baadhi ya mastaa hao kuondoka wakimuacha.

Habari za SimbaUjio wa kocha Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ulikuwa na furaha kwa mashabiki wa Simba lakini ni kama aliwakata vaibu alivyoshuhudia mechi ya Simba kwa mara ya kwanza pale visiwani Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi na kumtaja Kibu kama moja ya wachezaji alioridhishwa na ubora wake.

Kauli hiyo iliwachanganya mashabiki wa soka nchini, lakini huenda hawakumuelewa kwani baada ya hapo alitolea ufafanizi kauli ile akimtaja Kibu kama mchezaji mwenye sifa za aina yake.

“Kibu ni mchezaji tofauti na wengi kikosini, anaweza kushambulia, anaweza kukaba ana nguvu na pumzi ya kutosha na anaweza kucheza maeneo zaidi ya matatu uwanjani, sio wachezaji wote kikosini wana sifa hizo,” alisema Robertinho.

Baada ya hapo Kibu akawa panga pangua ndani ya kikosi cha Simba na kuwa na mchango mkubwa kwa safu ya ushambuliaji iliyojaa mafundi pia kwa safu ya ulinzi akisifika kwa kushambulia na kukaba.

Pamoja na yote hayo, Kibu hakuishia hapo kwani aliendelea kuamini katika mchakato wake na kujitafuta ndani ya Simba na Jumapili iliyopita ni kama alijipata baada ya kufunga bao la pili dhidi kwa timu yake wakati Simba ikiwaadhibu watani wao wa jadi, Yanga mabao 2-0.

HIZI HAPA KLABU 10 ZENYE THAMANI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI...CHAMA LAKO NAMBA NGAPI?Bao hilo la Kibu ndiyo habari ya mjini hadi leo kutokana na namna alivyolifunga lakini kubwa zaidi ni kufunga kwenye mechi ya Simba na Yanga yenye hisia, mvutu na mvutano mkubwa baina ya timu hizo mbili.

Baada ya bao hilo, majina mabaya kwa Kibu yaliufutwa na kupachikwa mazuri, kejeli, masimango na kumbeza havijaoneka tena zaidi ya kummwagia sifa kedekede na kila zuri lilikuwa upande wake na yeye ni kama alifahamu hilo litatokea kwani baada ya kufunga alishangilia kwa staili mbalimbali ikiwemo kuziba mdomo kwa kidole ishara ya kunyamazisha watu.

Akizungumza  Kibu alisema anafahamu kila kitu kinachoendelea juu yake lakini huwa hajali sana zaidi ya kupotezea na kufanya kazi yake ambayo ni kucheza tu.

“Mambo kama hayo yapo kwenye soka na mimi sio wa kwanza kutokea kwangu lakini naamini katika mimi na nikifanyacho hivyo huwa siyachukulii kwa ukubwa bali najitahidi kufanya vizuri kazi yangu na kwa juhudi ili kufikia malengo,” alisema Kibu mwenye mabao mawili hadi sasa kwenye ligi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI