News

TAA YA KIJANI YAMWAKIA KIBU DENIS….KUPIGWA BEI ULAYA …MAGORI AFUNGUKA DILI LOTE A-Z…

admin December 30, 2021 5:00 pm


UWEZO mkubwa aliouonyesha straika wa Simba, Kibu Denis na kufanikiwa kufunga mabao mawili dhidi ya KMC, umemuibua Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori ambaye ameweka wazi kuwa siku siyo nyingi straika huyo atauzwa Ulaya.

Kibu Ijumaa iliyopita alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara pale Simba walipoibuka wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC ambapo Kibu alifanikiwa kufunga mabao mawili.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili la mwezi Agosti mwaka huu akitokea ndani ya kikosi cha Mbeya City.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatatu, Magori alisema: “Binafsi sijashangazwa sana na kile ambacho amekifanya Kibu katika mchezo wetu uliopita dhidi ya KMC, kwa kuwa ni mchezaji ambaye nimekuwa nikimfuatilia tangu akiwa Geita na Mbeya City hivyo najua ubora mkubwa alionao.

“Huu ni miongoni mwa usajili bora ambao tumeufanya msimu huu, ni kweli bado kuna vitu anapaswa kuongezewa ili awe bora zaidi kuendana na mahitaji ya timu, lakini naamini siku sio nyingi tutaanza kupokea ofa kubwa kutoka Afrika na hata Ulaya kwa ajili ya Kibu.”

KIWANGO CHA LUIS MUQUISSONE CHAWALIZA MASHABIKI AL AHLY…WADAI NI HASARA KWA TIMU… KUHUSU ISHU YA PETER BANDA KUTIMKIA SAUDI ARABIA…UONGOZI SIMBA WATOA NENO..BARUA YAPOKELEWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply